Podcasts · Religion & Spirituality

Neno la Leo

Neno la Leo 255

126 episodes

Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana (Zaburi 118:24). Anza siku mpya ya Yesu kwa kusiliza na kutafakari nasi “Neno la Leo” kila siku kwa lugha ya Kiswahili.

Episodes page 1 of 3

  1. Kumbuka Mikono Iliyokushika Ulipokuwa Unaanguka!

    · 9:12 · S4 E28

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 19:31–39 tunakutana tena na Barzilai, mmoja wa watu waliomsaidia Mfalme Daudi alipokuwa amekimbia Yerusalemu kutokana na uasi wa mwanawe Absalomu. Unamkumbuka Barzilai?…

  2. Usitumie Nafasi Yako Kulipiza Kisasi cha Zamani!

    · 22 min · S4 E27

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 19:18–23 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kurudi baada ya uasi wa mwanawe Absalomu. Katika safari hiyo, Daudi anakutana tena na Shimei.…

  3. Hata Baada ya Kupoteza, Bado Unaweza Kuanza Upya!

    · 17 min · S4 E26

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 19:14–15 tunafika katika hatua mpya ya safari ya Mfalme Daudi. Baada ya kukimbia Yerusalemu kutokana na uasi wa mwanawe Absalomu, kupitia vita na hatimaye kumpoteza…

  4. Unaweza Kuwa Unaumia, Lakini Bado Kuna Wanaokuhitaji!

    · 7:39 · S4 E25

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 19:5–7 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi baada ya kifo cha mwanawe Absalomu. Jana tulimwona Daudi akilia kwa uchungu baada ya kupata taarifa kwamba mwanawe…

  5. Kuna Maumivu Ambayo Maneno Hayawezi Kuponya!

    · 20 min · S4 E24

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 18:31–33 tunafika katika moja ya sehemu zenye huzuni kubwa katika maisha ya Mfalme Daudi. Vita dhidi ya Absalomu vimekwisha. Jeshi la Daudi limeshinda na ufalme wake…

  6. Hatari ya Kiburi!

    · 18 min · S4 E23

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 18:9 tunaendelea na simulizi ya Absalomu wakati vita kati ya jeshi lake na jeshi la baba yake, Daudi, vinaendelea. Absalomu, kijana aliyekuwa amejenga ushawishi mkubwa…

  7. Hata Katika Migogoro, Upendo Unaweza Kubaki!

    · 7:18 · S4 E22

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 18:5 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu wakati vita kati ya majeshi yao vinapoanza. Kabla jeshi la Daudi halijaondoka kwenda vitani, Daudi anawaagiza…

  8. Usiwe Tu Unangoja Msaada, Kuwa Msaada kwa Wengine!

    · 10 min · S4 E21

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 17:27–29 tunamkuta Daudi akiwa Mahanaimu baada ya kukimbia Yerusalemu kutokana na uasi wa mwanawe Absalomu. Daudi na watu wake wamechoka, wana njaa na wana kiu. Hawajui…

  9. Mungu Hajakaa Kimya Kama Unavyofikiri!

    · 13 min · S4 E20

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 17:14 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu. Absalomu anatafuta ushauri wa namna ya kumshinda baba yake. Ahithofeli anatoa mpango wa kumshambulia Daudi…

  10. Unaweza Kumjibu, Lakini Je, Ni Lazima?

    · 15 min · S4 E19

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 16:5–12 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya uasi wa mwanawe Absalomu. Daudi tayari anapitia kipindi kigumu.…

  11. Imani ya Kweli Haitegemei Jibu Unalotaka!

    · 12 min · S4 E18

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:25–26 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya uasi wa mwanawe Absalomu. Katika safari hiyo, makuhani wanakuja…

  12. Si Kila Anayekufuata Wakati wa Furaha Atasimama Nawe Wakati wa Shida!

    · 20 min · S4 E17

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:19–21 tunaendelea na simulizi ya Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya mwanawe Absalomu kuanza kuuchukua ufalme. Katika hali hii ya kutokuwa na…

  13. Mafanikio Hayamaanishi Mwisho wa Changamoto!

    · 18 min · S4 E16

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:13–14 tunamkuta Mfalme Daudi katika hali ambayo huenda hakuwahi kufikiria angeipitia tena. Miaka mingi iliyopita alikuwa akikimbia kutoka kwa Sauli. Lakini sasa…

  14. Tatizo Unalolipuuza Leo Linaweza Kukugharimu Kesho!

    · 22 min · S4 E15

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:10–12 tunaendelea na simulizi ya Absalomu, mwana wa Mfalme Daudi. Jana tulimwona akijenga ushawishi na kuiba mioyo ya watu wa Israeli. Leo mambo yamefika mbali…

  15. Usiishi Kwa Kutafuta Approval ya Watu!

    · 16 min · S4 E14

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 15:1–6 tunaendelea na simulizi ya Absalomu, mwana wa Mfalme Daudi. Baada ya kurudishwa Yerusalemu na hatimaye kukutana na baba yake, tunamwona Absalomu akianza kujenga…

  16. Si Kila “Tuko Sawa” Inamaanisha Tuko Sawa!

    · 10 min · S4 E13

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:32–33 tunamwona Absalomu hatimaye akikutana na baba yake, Mfalme Daudi, baada ya miaka mingi ya utengano. Absalomu anainama mbele ya baba yake na Daudi anambusu.…

  17. Sio Kila Ukimya Ni Amani!

    · 8:46 · S4 E12

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:28 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu. Biblia inatuambia kwamba Absalomu aliishi Yerusalemu kwa miaka miwili bila kuuona uso wa baba yake. Miaka…

  18. Si Kila Anayerudi Amerudishiwa Nafasi Moyoni!

    · 16 min · S4 E11

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:21–24 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu. Baada ya miaka ya utengano na mipango ya Yoabu, hatimaye Daudi anakubali Absalomu arudi Yerusalemu. Kwa…

  19. Si Kila Tatizo Jawabu Lake Ni Ukimya!

    · 17 min · S4 E10

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 14:1–3 tunaendelea na simulizi ya familia ya Daudi ambayo imepitia maumivu, ukatili, kisasi na sasa utengano. Baada ya Absalomu kumuua Amnoni, anakimbia na kuishi mbali…

  20. Kisasi Hakiponyi Jeraha!

    · 10 min · S4 E9

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:28–29 tunaendelea na simulizi ya familia ya Daudi, ambako maumivu ambayo hayajashughulikiwa sasa yanazaa maumivu mengine. Jana tulimwona Absalomu akiwa amebeba…

  21. Hatari ya Ukimya!

    · 18 min · S4 E8

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:21–22 tunaendelea na simulizi ngumu ya familia ya Daudi. Jana tulimwona Tamari akiwa amevunjika baada ya kile Amnoni alichomfanyia. Leo tunaona kile kinachotokea…

  22. Usipuuze Maumivu ya Aliyejeruhiwa!

    · 13 min · S4 E7

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:19–20 tunabaki katika simulizi ngumu ya Tamari. Jana tuliona ukatili ambao Amnoni alimfanyia. Leo Biblia haitukimbizi haraka kwenda kwenye tukio jingine.…

  23. Upendo wa Kweli Huheshimu Mipaka!

    · 9:30 · S4 E6

    🎙️ Leo katika Neno la Leo tunatafakari 2 Samweli 13:10–14, sehemu nzito na yenye maumivu katika simulizi la familia ya Daudi. Amnoni anapokuwa peke yake na Tamari anajaribu kumlazimisha kutimiza tamaa yake. Tamari…

  24. Usilishe Tamaa Isiyofaa Moyoni

    · 19 min · S4 E5

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 13:1–2 tunaingia katika sehemu ngumu na yenye huzuni katika familia ya Daudi. Tunamkuta Amnoni akianza kuwa na tamaa isiyofaa kwa Tamari, dada yake wa kambo. Lakini…

  25. Mungu Bado Anaweza Kuandika Sura Mpya!

    · 17 min · S4 E4

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:24–25 tunafika katika sehemu tofauti kabisa ya simulizi la Daudi. Tumemwona akikosea vibaya. Tumemwona akikubali dhambi yake. Tumemwona akisamehewa lakini…

  26. Baada ya Siku Ngumu, Unaweza Kuinuka Tena

    · 11 min · S4 E3

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:20 tunakutana na Daudi baada ya kupokea jibu ambalo hakulitaka. Jana tulimwona akiwa chini, akifunga na kumwomba Mungu kwa ajili ya mtoto wake. Leo habari inafika:…

  27. Omba Hata Kama Hujui Mungu Atajibu Vipi!

    · 7:54 · S4 E2

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:16–17 tunamwona Daudi katika sehemu tofauti kabisa na jana. Jana alisimama mbele ya Nathani na kukubali: “Nimemkosea Bwana.” Leo yuko chini mbele za Mungu akiomba.…

  28. Ukikosea, Usijifiche. Rudi kwa Mungu!

    · 15 min · S4 E1

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 2 Samweli 12:13–14 tunakutana na moja ya moments nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Nabii Nathani amesimama mbele yake na kumwambia wazi: “Wewe ndiye mtu huyo.” Daudi sasa…

  29. Maliza Vizuri!

    · 24 min · S3 E61

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:23–26 na 31:1–4 tunafunga mwezi wetu na wakati huohuo tunafika mwisho wa safari yetu kupitia kitabu cha 1 Samweli. Na Biblia inatuacha na picha mbili tofauti sana:…

  30. Mungu Anaweza Kukurejeshea Ulichofikiri Kimepotea!

    · 16 min · S3 E60

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:8, 18–19 tunaendelea na Daudi baada ya moja ya siku ngumu zaidi katika maisha yake. Jana tulimwacha Ziklagi ikiwa imechomwa moto. Familia zimechukuliwa mateka. Watu…

  31. Unaweza Kulia na Bado Ukawa na Imani!

    · 13 min · S3 E59

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 30:3–6 tunakutana na moja ya siku nzito zaidi katika maisha ya Daudi. Daudi na watu wake wanarudi Ziklagi wakitarajia kurudi nyumbani. Lakini wanapofika, wanakuta mji…

  32. Usifanye Maamuzi Makubwa Ukiwa Umechoka na Kuogopa!

    · 22 min · S3 E58

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 27:1 tunakutana na Daudi katika hali ambayo huenda wengi wetu tunaifahamu. Jana alikuwa amesimama imara katika imani. Alikuwa na nafasi nyingine ya kumuua Sauli lakini…

  33. Usijilipizie Kisasi Hata Ukipewa Nafasi

    · 8:35 · S3 E57

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 26:9–11 tunamwona Daudi akikabiliwa tena na mtihani ambao tayari aliwahi kuupita. Mara ya kwanza Sauli aliingia katika pango ambamo Daudi alikuwa amejificha. Daudi…

  34. Si Kila Anayekuzuia Ni Adui Yako!

    · 17 min · S3 E56

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 25:32–33 tunakutana na jambo la kushangaza kuhusu Daudi. Jana tulimwona akikataa kulipiza kisasi kwa Sauli. Lakini leo Daudi mwenyewe anakaribia kufanya kile…

  35. Usiruhusu Aliyekuumiza Abadilishe Wewe Ni Nani!

    · 19 min · S3 E55

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Kupitia 1 Samweli 24:12 tunaendelea na Daudi baada ya kukataa kumuua Sauli pangoni. Daudi anatoka nje na kumwonyesha Sauli kipande cha vazi lake. Ujumbe ni wazi: “Nilikuwa na nafasi ya…

  36. Si Kila Mlango Uliofunguka Ni Mlango wa Mungu!

    · 22 min · S3 E54

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Kupitia 1 Samweli 24:4–6 tunamwona Daudi akikabiliwa na nafasi ambayo kwa macho ya kibinadamu inaonekana kama jibu la maombi yake. Sauli amekuwa akimtafuta ili kumuua. Lakini sasa, bila…

  37. Kuwa Mtu Anayeimarisha Imani ya Wengine

    · 18 min · S3 E53

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 23:16 tunakutana tena na Yonathani. Daudi bado anakimbia. Sauli bado anataka kumuua na mazingira yake bado hayajabadilika. Lakini Yonathani anamtafuta Daudi. Na Biblia…

  38. Usifikiri Mungu Amekuacha Kwa Sababu Tatizo Bado Lipo

    · 11 min · S3 E52

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 23:14 tunamkuta Daudi bado anakimbia. Sauli hajakata tamaa. Maandiko yanasema alikuwa akimtafuta Daudi kila siku. Lakini katikati ya simulizi hiyo kuna maneno machache…

  39. Muulize Mungu Kabla ya Kuchukua Hatua!

    · 18 min · S3 E51

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 23:2 tunamwona Daudi akikabiliwa na uamuzi mwingine muhimu. Anaambiwa kwamba Wafilisti wanashambulia Keila na kuiba mazao yao. Daudi alikuwa na sababu nyingi za…

  40. Usihitimishe Hadithi Yako Ukiwa Pangoni!

    · 13 min · S3 E50

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 22:1–2 tunamkuta Daudi mahali ambapo huenda hakuwahi kufikiria angefika: katika pango la Adulamu. Fikiria safari yake. Alipakwa mafuta kuwa mfalme. Akamshinda Goliathi.…

  41. Hata Watu wa Imani Huogopa!

    · 35 min · S3 E49

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 21:12–13 tunakutana na upande tofauti kabisa wa Daudi. Huyu ndiye Daudi aliyesimama mbele ya Goliathi wakati jeshi lote la Israeli limejaa hofu. Huyu ndiye aliyesema,…

  42. Rafiki Yako Akifanikiwa Kuliko Wewe, Bado Utamshangilia?

    · 35 min · S3 E48

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 20:17 tunaendelea kuangalia urafiki wa ajabu kati ya Daudi na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba Yonathani alimpenda Daudi kama alivyoipenda nafsi yake mwenyewe na…

  43. Rafiki wa Kweli Anakutetea Hata Usipokuwepo!

    · 36 min · S3 E47

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 19:4–5 tunamwona Yonathani akifanya jambo linalotuonyesha maana nyingine ya urafiki wa kweli. Sauli sasa anataka Daudi auawe. Daudi hayupo kwenye mazungumzo haya lakini…

  44. Unaweza Kufanikiwa Bila Kumpoteza Mungu Njiani!

    · 22 min · S3 E46

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 18:14 tunakutana na maneno machache lakini yenye ujumbe mkubwa sana kuhusu maisha ya Daudi: “Daudi akafanikiwa katika njia zake zote, naye Bwana alikuwa pamoja naye.”…

  45. Usiruhusu Wivu Uharibu Moyo Wako!

    · 35 min · S3 E45

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 18:7–9 tunaona mabadiliko ya kusikitisha yakianza ndani ya moyo wa Sauli. Baada ya ushindi, wanawake wanaimba wakisema Sauli amewaua maelfu yake na Daudi makumi ya…

  46. Mungu Hutupa Watu wa Kutembea Nasi!

    · 53 min · S3 E44

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 18:1–3 tunaanza kuona maisha ya Daudi baada ya ushindi dhidi ya Goliathi. Lakini jambo la kwanza tunalokutana nalo si vita nyingine. Tunakutana na Yonathani. Maandiko…

  47. Usidharau Kile Mungu Amekiweka Mikononi Mwako!

    · 44 min · S3 E43

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:49–50 tunafika katika wakati ambao tumekuwa tukiuelekea kwa siku kadhaa. Daudi anaweka mkono katika mfuko wake, anachukua jiwe, analitia katika kombeo na kumpiga…

  48. Fanya Unachoweza, Mungu Atashughulikia Usichoweza!

    · 23 min · S3 E42

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:47 tunaendelea pale tulipoishia jana. Daudi amemwambia Goliathi, “Ninakujia kwa jina la Bwana.” Sasa anaongeza jambo muhimu zaidi: “Vita ni vya Bwana.” Lakini…

  49. Kwa Jina la Bwana!

    · 14 min · S3 E41

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:45 tunafika katika moja ya kauli zenye nguvu zaidi katika simulizi ya Daudi na Goliathi. Goliathi anasimama mbele ya Daudi akiwa na upanga, fumo, mkuki, uzoefu wa…

  50. Usijaribu Kuwa Mtu Mwingine!

    · 40 min · S3 E40

    🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 17:38–40 tunaendelea na simulizi ya Daudi kuelekea kwa Goliathi. Baada ya Sauli kukubali Daudi aende kupigana, anamvika mavazi yake ya vita, kofia ya shaba, deraya na…

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.