Podcasts Β· Neno la Leo

Si Kila Anayerudi Amerudishiwa Nafasi Moyoni!

Β· 16 min Β· S4 E11

Episode Si Kila Anayerudi Amerudishiwa Nafasi Moyoni!

0:00 15:55

πŸŽ™οΈ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 2 Samweli 14:21–24 tunaendelea na simulizi ya Daudi na mwanawe Absalomu.

Baada ya miaka ya utengano na mipango ya Yoabu, hatimaye Daudi anakubali Absalomu arudi Yerusalemu.

Kwa juu juu, hizi zinaonekana kuwa habari njema.

Mwana anarudi nyumbani.

Lakini kuna jambo la kushangaza.

Daudi anasema:

β€œNa ageukie nyumbani kwake wala asiuone uso wangu.”

Kwa hiyo Absalomu anarudi Yerusalemu lakini haruhusiwi kukutana na baba yake.

Wako mji mmoja.

Lakini mioyo yao bado iko mbali.

Na hapa tunapata somo muhimu sana:

Kuwa karibu sio sawa na kupatana.

Wakati mwingine tunafikiri kwamba watu wakirudiana au wakianza kukaa pamoja tena, basi matatizo yao yameisha.

Lakini si lazima iwe hivyo.

Unaweza kuwa kwenye ndoa moja lakini hamzungumzi kuhusu mambo yanayowaumiza.

Unaweza kuwa nyumba moja na ndugu yako lakini kuna uchungu ambao haujawahi kushughulikiwa.

Unaweza kufanya kazi na mtu kila siku, mnasalimiana na hata kucheka pamoja lakini ndani kuna jambo ambalo hakuna anayethubutu kulizungumzia.

Proximity is not reconciliation.

Ukaribu wa kimwili hauhakikishi ukaribu wa mioyo.

Na hilo ndilo tunaloliona kwa Daudi na Absalomu.

Daudi ameruhusu mwanawe arudi lakini bado hajaweka mazingira ya mazungumzo na upatanisho wa kweli.

Absalomu amerudi nyumbani lakini bado kuna umbali kati yake na baba yake.

Mahali pamebadilika lakini tatizo la msingi bado lipo.

Na huenda hata sisi tunafanya hivyo katika mahusiano yetu.

Tunamwambia mtu, β€œSawa, turudiane.”

Lakini hatuzungumzi kuhusu kile kilichotutenganisha.

Tunasema, β€œYameisha.”

Lakini ndani ya moyo bado kuna maswali, maumivu na uchungu.

Tunajaribu kurudisha mambo kama zamani bila kushughulikia kilichoharibika.

Wakolosai 3:13 inatuita kuvumiliana na kusameheana.

Na Waefeso 4:15 inatufundisha kusema kweli katika upendo.

Kwa sababu upatanisho wa kweli unahitaji zaidi ya kuwa karibu.

Unahitaji ukweli.

Unahitaji kusikilizana.

Unahitaji kukubali makosa na kuwajibika.

Unahitaji msamaha na pale ambapo uaminifu umevunjika, mara nyingi unahitaji muda na matendo yanayojenga trust tena.

Na katika mahusiano ambayo kumekuwa na ukatili au madhara makubwa, upatanisho haupaswi kulazimishwa kwa gharama ya usalama wa aliyeumizwa.

Kuwa na amani na mtu hakumaanishi lazima urudi kwenye mazingira yasiyo salama.

Lakini pale ambapo upatanisho unawezekana, tusiridhike na ukaribu wa nje huku mioyo ikiwa mbali.

Leo jiulize:

Je, kuna mtu ambaye tuko karibu kimwili lakini bado kuna umbali mkubwa kati ya mioyo yetu?

Huenda tunaishi pamoja lakini hatuelewani.

Huenda tunazungumza kila siku lakini hatujawahi kushughulikia kile kilichotuumiza.

Huenda tumesema tumesameheana lakini bado hatujajenga upya uaminifu.

Kumbuka:

Kurudisha mtu karibu sio sawa na kurejesha mahusiano.

Na wakati mwingine, hatua muhimu zaidi si kumwambia mtu, β€œRudi.”

Ni kuwa tayari kuuliza:

β€œNi nini kilituvunja na tunawezaje kuanza kushughulikia jambo hilo kwa ukweli na upendo?”

Kwa sababu mwisho wa siku, si muhimu tu kwamba tuko sehemu moja. Ni muhimu pia kujua kama mioyo yetu imeanza kupona.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. πŸ™πŸ“–βœ¨

The episode on the publisher’s site (opens in a new tab)

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.