Usifikiri Mungu Amekuacha Kwa Sababu Tatizo Bado Lipo
· 11 min · S3 E52
Episode Usifikiri Mungu Amekuacha Kwa Sababu Tatizo Bado Lipo
🎙️ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 1 Samweli 23:14 tunamkuta Daudi bado anakimbia. Sauli hajakata tamaa. Maandiko yanasema alikuwa akimtafuta Daudi kila siku.
Lakini katikati ya simulizi hiyo kuna maneno machache yenye ujumbe mkubwa sana:
“Lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.”
Angalia jambo hilo. Mungu hakumwondoa Sauli mara moja. Hakumaliza tatizo lote siku hiyo. Daudi bado alikuwa jangwani. Bado alikuwa anahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Bado kulikuwa na hatari na uncertainty.
Lakini Mungu alikuwa anamshikilia katikati ya hayo yote.
Mara nyingi tunafikiri ulinzi wa Mungu lazima uonekane kwa tatizo kuondoka. Tunaomba, “Bwana, niondolee hili.” Na wakati mwingine Mungu huliondoa. Lakini kuna nyakati tatizo haliondoki mara moja na Mungu anatufundisha kuona kwamba uwepo wa tatizo si ushahidi wa kutokuwepo kwake.
Huenda bado hujapata jibu ulilokuwa unasubiri. Huenda bado unapambana na jambo lilelile. Huenda mazingira yako hayajabadilika kwa namna uliyotarajia.
Lakini ukiangalia safari yako vizuri, huenda ukaona jambo jingine: tatizo halikuondoka mara moja lakini Mungu hakukuacha.
Daudi alikuwa amepakwa mafuta kuwa mfalme lakini bado alikuwa jangwani. Sauli alikuwa na jeshi na alikuwa akimtafuta kila siku. Lakini Sauli hakuweza kumaliza kile ambacho Mungu alikuwa bado anakijenga ndani ya Daudi.
Na huenda huo ndio ushuhuda wako pia.
Wakati mwingine ushuhuda si, “Mungu aliondoa tatizo mara moja.”
Wakati mwingine ushuhuda ni:
“Nilipitia jambo ambalo nilifikiri lingenimaliza, lakini Mungu akanishikilia mpaka nikapita.”
Kwa hiyo usihitimishe kwamba Mungu hayupo kwa sababu tu Sauli bado anakutafuta.
Tatizo linaweza kuwa bado lipo. Lakini Mungu bado yupo.
Na wakati mwingine muujiza si kwamba tatizo liliondoka.
Muujiza ni kwamba tatizo halikuweza kukuondoa wewe.
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨
Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.