Imani ya Kweli Haitegemei Jibu Unalotaka!
Β· 12 min Β· S4 E18
Episode Imani ya Kweli Haitegemei Jibu Unalotaka!
ποΈ Leo kwenye Neno la Leo
Leo kupitia 2 Samweli 15:25β26 tunaendelea na simulizi ya Mfalme Daudi akiwa katika safari ya kukimbia Yerusalemu baada ya uasi wa mwanawe Absalomu.
Katika safari hiyo, makuhani wanakuja wakiwa wamebeba Sanduku la Agano. Lakini Daudi anawaambia walirudishe Yerusalemu.
Kisha anasema maneno yenye uzito mkubwa:
βKama nikipata kibali machoni pa Bwana, atanirudisha tena.β
Lakini anaendelea kusema kwamba kama Mungu hatapendezwa naye, basi afanye kile anachoona kuwa chema.
Daudi hajaribu kutumia Sanduku la Agano kama guarantee ya ushindi. Hajaribu kumlazimisha Mungu amrudishe kwenye kiti cha enzi.
Anamkabidhi Mungu hata matokeo ya safari yake.
Na hapa tunajifunza jambo muhimu kuhusu imani.
Mara nyingi tunamwomba Mungu atufungulie milango, atufanikishe na atujibu kwa namna tunayotamani.
Lakini je, bado tutamwamini kama jibu lake litakuwa tofauti?
Yesu mwenyewe katika Luka 22:42 aliomba:
βSi mapenzi yangu, bali yako yatendeke.β
Imani ya kweli si kumwamini Mungu kwa sababu tuna uhakika atafanya kila tunachotaka.
Ni kumwamini kwa sababu tunajua yeye ni mwaminifu hata wakati hatujui atakachofanya.
Kwa hiyo leo jiulize:
Je, ninamkabidhi Mungu mipango yangu pekee au niko tayari kumkabidhi pia matokeo yake?
Kwa sababu wakati mwingine sala ya imani si kusema, βBwana, lazima hili litokee.β
Ni kusema:
βBwana, hiki ndicho ninachotamani. Lakini zaidi ya matakwa yangu, mapenzi yako yatimizwe.β
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. ππβ¨
Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.