Podcasts Β· Neno la Leo

Rafiki Yako Akifanikiwa Kuliko Wewe, Bado Utamshangilia?

Β· 35 min Β· S3 E48

Episode Rafiki Yako Akifanikiwa Kuliko Wewe, Bado Utamshangilia?

0:00 35:27

πŸŽ™οΈ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 20:17 tunaendelea kuangalia urafiki wa ajabu kati ya Daudi na Yonathani. Maandiko yanatuambia kwamba Yonathani alimpenda Daudi kama alivyoipenda nafsi yake mwenyewe na akamtaka athibitishe tena kiapo chao.

Lakini kuna kitu kinachoufanya urafiki huu kuwa wa kipekee zaidi.

Yonathani alikuwa mwana wa mfalme. Kwa kawaida angeweza kutarajia kwamba siku moja angechukua nafasi ya baba yake. Lakini kadiri Daudi anavyosogea katika kusudi la Mungu juu ya maisha yake, ndivyo uwezekano wa Yonathani kuwa mfalme unavyopungua.

Yonathani angeweza kumwangalia Daudi na kuona competitor. Badala yake, alimwona rafiki.

Na hapo ndipo urafiki unapopimwa.

Ni rahisi kumshangilia rafiki yako anapoanza biashara. Lakini biashara yake ikianza kufanya vizuri kuliko yako je? Ni rahisi kumpongeza anapopata nafasi nzuri. Lakini akipata nafasi ambayo wewe pia uliitamani je? Ni rahisi kufurahia maendeleo ya mtu mpaka maendeleo yake yanapoanza kugusa eneo ambalo wewe pia ulitamani kufanikiwa.

Watu wengi wanaweza kushangilia ushindi wako mpaka ushindi wako uanze kugusa nafasi yao.

Lakini Yonathani anatufundisha kwamba rafiki si competitor wako kwa sababu tu Mungu anafanya jambo kubwa katika maisha yake. Baraka yake haimaanishi kushindwa kwako.

Dunia inatufundisha kuuliza, β€œMtu huyu anaweza kunisaidiaje?” Urafiki wa kweli unauliza, β€œNinawezaje kuwa mwaminifu kwake hata kama hakuna faida ninayopata?”

Na huenda leo tunahitaji kujiuliza swali gumu kidogo:

Rafiki yangu akifanikiwa kuliko mimi, bado nitaweza kumshangilia kwa moyo safi?

Kwa sababu upendo wa kweli hauishii pale mafanikio ya mwingine yanapoanza kutugharimu. Yonathani hakumgeuza Daudi kuwa mshindani kwa sababu tu Mungu alikuwa akimwinua.

Huo ndio moyo tunaohitaji: moyo unaoweza kusema, β€œKama Mungu anakufungulia mlango, nitafurahi pamoja nawe. Sitafanya baraka yako kuwa tishio kwangu.”

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. πŸ™πŸ“–βœ¨

The episode on the publisher’s site (opens in a new tab)

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.