Podcasts Β· Neno la Leo

Israeli Walishindwa, Lakini Mungu Hakushindwa!

Β· 23 min Β· S3 E14

Episode Israeli Walishindwa, Lakini Mungu Hakushindwa!

0:00 23:26

πŸŽ™οΈ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 5:3–4 tunaendelea na simulizi ya Sanduku la Agano baada ya kutekwa na Wafilisti. Wanalichukua na kuliweka katika hekalu la Dagoni kana kwamba ushindi wao dhidi ya Israeli ulimaanisha kuwa mungu wao alikuwa amemshinda Mungu wa Israeli. Lakini asubuhi Dagoni anakutwa ameanguka chini mbele ya Sanduku. Wanamwinua na siku inayofuata anaanguka tena, safari hii kichwa na mikono yake ikiwa imekatwa. Ujumbe ni mzito: Israeli walikuwa wameshindwa vita lakini Mungu wao hakuwa ameshindwa. Neno la leo linatukumbusha kwamba hata tunapopitia kushindwa, kupoteza au mazingira yanayoonekana kuwa nje ya uwezo wetu, tusifikiri kwamba Mungu amepoteza mamlaka yake. Je, kuna β€œDagoni” katika maisha yako ambayo imeonekana kubwa kiasi cha kukufanya uogope? Kumbuka, kile kinachokushinda wewe hakiwezi kumshinda Mungu.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. πŸ™πŸ“–βœ¨

The episode on the publisher’s site (opens in a new tab)

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.