Subiri kwa Amani, Kisha Mpe Mungu Utukufu!
ยท 18 min ยท S3 E5
Episode Subiri kwa Amani, Kisha Mpe Mungu Utukufu!
๐๏ธ Leo kwenye Neno la Leo
Leo tunahitimisha simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:27โ28. Baada ya kusubiri kwa imani na kupokea amani kabla ya jibu, Hana anashuhudia uaminifu wa Mungu na anarudi mbele zake kutimiza ahadi yake. Hakuliona jibu la maombi yake kama mafanikio yake binafsi bali kama zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo akamrudishia Mungu kile alichokuwa amempa. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba kusubiri si kipindi cha kupoteza muda bali ni kipindi ambacho Mungu hutufundisha kumtumaini. Na anapojibu maombi yetu, tusiishie kufurahia baraka bali turudi kwake kwa moyo wa shukrani na kumtukuza. Je, tunamtafuta Mungu kwa ajili ya zawadi zake pekee au tuko tayari kumheshimu na kumwabudu hata baada ya kupokea tulichokiomba?
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. ๐๐โจ
Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.