Mungu Hukupa Amani Kwanza Kabla ya Majibu!
Β· 14 min Β· S3 E3
Episode Mungu Hukupa Amani Kwanza Kabla ya Majibu!
ποΈ Leo kwenye Neno la Leo
Leo tunaendelea na simulizi ya Hana kupitia 1 Samweli 1:17. Baada ya kumimina moyo wake mbele za Mungu, Hana anapokea maneno ya kuhani Eli: βNenda kwa amani.β Cha kushangaza ni kwamba hali yake ilikuwa bado haijabadilika, lakini moyo wake ulikuwa umebadilika. Kupitia simulizi hii tunajifunza kwamba Mungu mara nyingi hutupa amani kabla ya kutupa jibu la maombi yetu. Tunapomkabidhi mizigo yetu kwa imani, tunaweza kuishi kwa utulivu hata wakati bado tunasubiri muujiza. Je, tunasubiri amani baada ya majibu, au tunaamini kwamba Mungu anaweza kutujaza amani hata kabla ya kuona kile tulichokiomba?
Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. ππβ¨
Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.