Podcasts ยท Neno la Leo

Kile Ulichopoteza Kinaweza Kukupeleka Kwenye Kusudi Lako!

ยท 19 min ยท S3 E21

Episode Kile Ulichopoteza Kinaweza Kukupeleka Kwenye Kusudi Lako!

0:00 18:53

๐ŸŽ™๏ธ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 9:6 tunaanza safari ya Sauli kwa tukio linaloonekana la kawaida kabisa. Punda wa baba yake wamepotea na Sauli anaondoka kwenda kuwatafuta. Lakini kile ambacho Sauli hajui ni kwamba wakati yeye anatafuta punda, Mungu anamwelekeza kuelekea kukutana na Samweli na kwenye hatua ambayo itabadilisha maisha yake kabisa.

Neno la leo linatukumbusha kwamba si kila safari tunayopitia tutaielewa tunapoianza. Wakati mwingine tunadhani tunatafuta kitu kimoja kumbe Mungu anatumia safari hiyo kutupeleka kwenye jambo ambalo hatukulitarajia. Hata usumbufu, kuchelewa au jambo ambalo halikuwa katika mipango yetu linaweza kuwa sehemu ya njia ambayo Mungu anaitumia kutupeleka mahali fulani.

Je, kuna jambo katika maisha yako leo ambalo halina maana kwako? Usiharakishe kuliona kama kupoteza muda. Sauli aliondoka nyumbani akitafuta punda waliopotea bila kujua kwamba Mungu alikuwa tayari amepanga kukutana kwake na Samweli. Wakati mwingine kile tunachokiita usumbufu, Mungu anaweza kuwa anakitumia kama direction kuelekea hatua inayofuata ya kusudi lake.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. ๐Ÿ™๐Ÿ“–โœจ

The episode on the publisher’s site (opens in a new tab)

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.