Podcasts ยท Neno la Leo

Hata Sasa Bwana Ametusaidia!

ยท 8:03 ยท S3 E17

Episode Hata Sasa Bwana Ametusaidia!

0:00 8:03

๐ŸŽ™๏ธ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 7:12 tunafika katika wakati wa ushindi baada ya Israeli kumrudia Mungu. Samweli anasimamisha jiwe na kuliita Ebeneza, akisema, โ€œHata hapa Bwana ametusaidia.โ€ Jiwe hilo lilikuwa ukumbusho kwamba hawakufika pale kwa nguvu zao wenyewe bali kwa msaada wa Mungu. Nasi tunapoitazama safari ya maisha yetu kuna milima tuliyodhani hatutaivuka, milango tuliyodhani haitafunguka na nyakati ambazo hatukujua tutafikaje kesho. Lakini leo tupo hapa. Neno la leo linatufundisha umuhimu wa kukumbuka uaminifu wa Mungu kwa sababu kumbukumbu ya kile Mungu alichotenda jana hutupa imani ya kumwamini kwa yale yaliyo mbele yetu. Je, unapoitazama safari yako unaweza kutambua Ebeneza zako na kusema, โ€œHata hapa Bwana amenisaidiaโ€? Kama Mungu amekuwa mwaminifu mpaka hapa, tunaweza kumtumainia pia katika hatua inayofuata.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. ๐Ÿ™๐Ÿ“–โœจ

The episode on the publisher’s site (opens in a new tab)

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.