Podcasts Β· Neno la Leo

Je, Unaweza Kumsubiri Mungu Wakati Kila Kitu Kinaenda Vibaya?

Β· 26 min Β· S3 E28

Episode Je, Unaweza Kumsubiri Mungu Wakati Kila Kitu Kinaenda Vibaya?

0:00 25:51

πŸŽ™οΈ Leo kwenye Neno la Leo

Leo kupitia 1 Samweli 13:13–14 tunaanza kuona ufa mkubwa katika uongozi wa Sauli. Wafilisti wanatishia Israeli, watu wanaanza kutawanyika na Samweli haonekani kufika kwa wakati ambao Sauli alitarajia. Akiwa chini ya presha, Sauli anaamua kuchukua hatua mwenyewe. Tatizo halikuwa kwamba hakufanya chochote. Tatizo ni kwamba alifanya jambo ambalo Mungu hakumwagiza kwa sababu hakuweza kusubiri.

Neno la leo linatukumbusha kwamba wakati mwingine presha ndiyo hufunua kina cha utiifu wetu. Ni rahisi kusubiri wakati kila kitu kiko sawa. Lakini je, tunaweza kuendelea kumtii Mungu wakati muda unaonekana kuisha, watu wanaondoka na mazingira yanatuambia, β€œFanya kitu sasa!”?

Hapa tunakumbushwa pia safari ya Hana tuliyoiona mwanzoni mwa 1 Samweli. Hana alijifunza kusubiri mpaka wakati wa Mungu ufike. Sauli anatuonyesha upande mwingine: kile kinachoweza kutokea tunaposhindwa kusubiri. Njia ya haraka si lazima iwe njia sahihi na kuchelewa tunakokiona si ruhusa ya kutangulia mbele ya Mungu.

Je, kuna jambo katika maisha yako ambalo presha inakusukuma kuliamua haraka? Kabla hujachukua hatua, jiulize: Ninaongozwa na Mungu au ninaongozwa na hofu kwamba muda wangu unaisha? Wakati mwingine tendo kubwa zaidi la imani si kufanya kitu haraka bali kuwa na subira ya kusubiri na kubaki katika utiifu.

Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. πŸ™πŸ“–βœ¨

The episode on the publisher’s site (opens in a new tab)

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them. Explicit shows are for adult profiles only, and children’s profiles hear only children’s shows. More about this list.