# Kumuheshimu Mungu ni Njia ya Kwenda Mbele!

An episode of [Neno la Leo](https://invisiblenetwork.ai/podcast/1896944111), 10 Aug 2026, 20 min.

Audio: https://content.rss.com/episodes/392262/3057023/neno-la-leo/2026_08_09_20_36_44_5432b2c9-97e6-4fa0-9032-5f829e973a2b.mp3

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 2:30 tunaingia katika simulizi ya familia ya Eli na kukutana na kanuni nzito kutoka kwa Mungu: “Wale wanaoniheshimu nitawaheshimu.” Wana wa Eli walikuwa na nafasi ya kuheshimiwa kama makuhani lakini walitumia nafasi hiyo vibaya na kuidharau kazi ya Mungu. Kupitia maisha yao tunajifunza kwamba mbele za Mungu cheo, nafasi au kuonekana wa kiroho hakutoshi. Kumheshimu Mungu kunaonekana katika namna tunavyoishi, tunavyotumia mamlaka tuliyopewa na maamuzi tunayofanya hata wakati hakuna anayetuona. Dunia inaweza kutupa heshima kwa sababu ya mafanikio yetu lakini kuna heshima nyingine inayotoka kwa Mungu mwenyewe. Je, maisha yetu yanamheshimu Mungu au tunataka Mungu atuheshimu wakati sisi hatumpi nafasi ya kwanza? Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them.
