# Usitafute Baraka Pekee, Tafuta Uwepo wa Mungu!

An episode of [Neno la Leo](https://invisiblenetwork.ai/podcast/1896944111), 12 Aug 2026, 19 min.

Audio: https://content.rss.com/episodes/392262/3061080/neno-la-leo/2026_08_11_13_50_18_f3917f18-883d-4ecc-86b0-a9838af16d75.mp3

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 3:19 tunaona Samweli akiendelea kukua na kuingia katika kusudi lake kama nabii. Lakini Biblia inatuonyesha siri iliyokuwa nyuma ya safari yake: “Bwana alikuwa pamoja na Samweli.” Mafanikio yake hayakuanzia katika kipawa, uwezo au nafasi yake bali katika uwepo wa Mungu uliokuwa pamoja naye. Hili linatufundisha kwamba tunaweza kuwa na mipango mizuri, elimu, fedha na watu sahihi lakini tusikose kile kilicho muhimu kuliko vyote: Mungu kuwa pamoja nasi. Swali letu lisibaki tu, “Bwana, utabariki mipango yangu?” bali pia, “Bwana, je, ninatembea pamoja nawe katika mipango hii?” Kwa sababu baraka kubwa kuliko kile Mungu anaweza kutupa ni uwepo wake katika safari yetu. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them.
