# Usimzoee Mungu Mpaka Ukasahau Utakatifu Wake!

An episode of [Neno la Leo](https://invisiblenetwork.ai/podcast/1896944111), 15 Aug 2026, 8:05.

Audio: https://content.rss.com/episodes/392262/3069284/neno-la-leo/2026_08_14_21_04_30_b2e3433c-4703-4ad4-88c9-65f7758aefe8.mp3

🎙️ Leo kwenye Neno la Leo Leo kupitia 1 Samweli 6:20 tunakutana na swali zito: “Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu mtakatifu?” Baada ya kuona jinsi Mungu alivyoonyesha nguvu zake dhidi ya Wafilisti, sasa Waisraeli wanakumbushwa kwamba Mungu si mwenye nguvu tu, Yeye ni mtakatifu. Neno la leo linatukumbusha kwamba tunaweza kumzoea Mungu kiasi cha kupoteza kicho na heshima tunayopaswa kuwa nayo mbele zake. Ni kweli Mungu ni Baba yetu na anatupenda lakini neema yake haijafanya dhambi kuwa jambo dogo wala utakatifu wake kupungua. Je, ukaribu wetu na Mungu umetufanya tumheshimu zaidi au tumemzoea kiasi kwamba mambo yake matakatifu yamekuwa ya kawaida kwetu? Mungu anatualika kuwa karibu naye lakini pia kutembea mbele zake kwa heshima, utiifu na utakatifu. Karibu tusikilize, tutafakari na kujifunza pamoja. 🙏📖✨

Shows are listed from Apple Podcasts' charts and directory, and Podcast Index where it is used. Every show and episode belongs to its publisher and plays from the publisher's own feed; this site hosts none of them.
